Man United kumtumia De Gea kumpata Bale??!!
Imeripotiwa kua Man United wanataka kumtumia
kipa wao David De Gea kama chambo kwenye jaribio lao la mwisho kumnasa Gareth Bale kutoka Real Madrid.
Mashetani hao wekundu wamekua wakihusishwa na nyota huyto kwa wiki kadhaa sasa ambapo kwa sasa wamekua wakionekana kutaka kuimarisha safu ya ushambuliaji kwa kuongeza mchchezaji mwingine.
Madrid wao wako tayari kumsaini De Gea ambaye hajacheza mechi yoyote Man United mpaka sasa kutokana na kile ambacho kocha van Gaal anadai kipa huyo hayuko sawa kwa sasa kiakili kutokana kuchanganywa na swala hili la kwenda Real madrid.
Kwa mujibu wa ESPN , kwa sasa Man United wanataka kutumia usajili wa De Gea kama kichocheo cha kuwafanya Real Madrid kukubali mazungumzo ya uhamisho wa Bale.
Hata hivyo bado hakuna dalili zozote za wazi ambazo zinaweza kuonesha Bale anataka kuondoka Santiago Bernabeu kbala ya kufungwa dirisha la usajili Jumanne ijayo.
Bale alisajiliwa Real Madrid kwa ada iliyovunja rekodi ya £85m mwaka 2013.
Man United kumtumia De Gea kumpata Bale??!!
Reviewed by Steve
on
Thursday, August 27, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment