Propellerads

Van Gaal: Schwensteiger alicheza vibaya




Meneja wa mashetani wekundu, Louis van Gaal amekosoa uchezaji wa nyota
mpya klabuni hapo Bastian Schwensteiger katika kipindi cha pili kwenye mechi dhidi ya San Jose Earthquakes ambapo hata hivyo Man United waliibuka na ushindi.

Mkali huyo kutoka Ujerumani alicheza dhidi ya San Jose jumanne usiku, ambayo inakua ni mechi yake ya pili tangu ajiunge klabuni hapo akitokea Bayern Munich wiki iliyopita.

Huku van Gaal akionekana kufurahia perfomance ya timu yake katika kipindi cha kwanza, lakini alionekana kuhitaji kasi zaidi katika kipindi cha pili kwenye mchezo huo walioshinda 3-1

Baada ya kuulizwa na waandishi ni jinsi gani alivyochukulia perfomance ya Schwensteiger katika kipindi cha pili, van Gaal alijibu "Amecheza vibaya pia, mchezaji unaweza kucheza vibaya, tena kama ukiwa umefanya mazoezi ndani ya siku tatu au sita, unahitaji kucheza dakika kama 45 hivi. Wengi wanadhani ni rahisi kuzoea, sio rahisi kiivo"

Man United watapambana na Barcelona Jumamosi hii huko California katika International Champions.


Van Gaal: Schwensteiger alicheza vibaya Van Gaal: Schwensteiger alicheza vibaya Reviewed by Steve on Wednesday, July 22, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.