La liga kuendelea kama kawa
Mahakama hiyo imeamua kuwa mgomo ulioitishwa na shirikisho la mchezo huo (RFEF) uliodumu kwa juma moja unakiuka vipengele vya
makubaliano ya upeperushaji wa mechi hizo.
(RFEF) iliiitisha mgomo kupinga sera mpya inayopendekezwa na serikali ya kudhibiti mikataba ya upeperushaji wa mechi za ligi hiyo maarufu.
Kauli hiyo ya mahakama inaruhusu mechi za ligi kuu zilizokuwa zimesalia kabla ya msimu kukamilika kuchezwa wikiendi hii.
Vinara wa soka ya Uhispania Barcelona watakuwa katika nafasi nzuri ya kutawazwa mabingwa iwapo watawacharaza mabingwa watetezi Atletico Madrid siku ya jumapili.
Aidha fainali ya kombe la mfalme huenda ikachezwa mwishoni mwa mwezi huu kufuatia uamuzi huo.
Barca, ambao tayari wamefuzu kwa fainali ya kombe la mabingwa barani ulaya ambapo wameratibiwa kukwaruzana na Juventus, watachuana dhidi ya Athletic Bilbao uwanjani Nou Camp katika fainali ya kombe la Mfalme ama Copa del Rey .
La liga kuendelea kama kawa
Reviewed by Steve
on
Friday, May 15, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, May 15, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment