Hiki ndio kikosi bora cha Julio VPL 2014/15
BAADA ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015 kumalizika mei 9 mwaka huu na Yanga wakiibuka mabingwa, vimejitokeza vikosi bora vilivyochaguliwa na makocha wa timu za ligi kuu na wasiokuwa na timu pamoja na wachambuzi wa soka nchini.
Jana kocha mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm alitaja kikosi ch kikosi bora cha VPL 2014/2015 nae kocha wa Coastal Union, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’. ana cha kwake
Katika mahojiano na mtandao huu Julio amesema kikosi chake bora kutokana na mechi za ligi kuu alizoziona ni:
- Ally Mustafa ‘Bartez’ (Yanga)
- Shomari Salum Kapombe (Azam fc)
- Paul Ngalema (Ndanda fc)
- Juma Nyosso (Mbeya City)
- Paschal Wawa (Azam fc)
- Jonas Mkude (Simba)
- Simon Msuva Yanga)
- Salum Telela (Yanga)
- Amissi Tambwe (Yanga)
- Ibrahim Ajib (Simba)
- Malim Busungu (Mgambo)
Kesho tutakuletea kikosi cha Kocha wa Mbeya City fc, Juma Mwambusi na kumbuka huyu ndiye kocha bora wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2013/2014 na msimu wa 2014/2015 uliomalizika mei 9 mwaka huu timu yake imeshika nafasi ya nne huku akitajwa kuwa miongoni mwa makocha wanaowania tuzo ya kocha bora kwa mara ya pili tena.
Hiki ndio kikosi bora cha Julio VPL 2014/15
Reviewed by Steve
on
Thursday, May 14, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, May 14, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment