Propellerads

Homa ya pambano, Yanga wajibiwa na Azam kwa staili hii...




Wakati Yanga wakienda kujificha Mbeya kwaajili ya maandalizi ya
ligi kuu na mechi ya Ngao ya Jamii, mabingwa wa Kombe la Afrika Mashariki na Kati ‘Kagame Cup’, Azam FC wanaondoka leo asubuhi kuelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya maandalizi zaidi.
 Azam FC inaingia msituni kujiwinda na mechi yao ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga itakayochezwa mwishoni mwezi huu kabla ya kuanza kwa mikikimikiki ya  ligi kuu Tanzania bara.
 Kocha mkuu wa kikosi hicho, Stewart Hall aliwapa mapumziko wachezaji wake mara tu baada ya kuchukua ubingwa huo uliowafanya waandike historia mpya kwani ni mara ya kwanza kwao kutwaa Kombe hilo pia walicheza bila kuruhusu bao hata moja langoni mwao.
Azam itacheza na Yanga mechi hiyo baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye ligi na Yanga ikiwa ni mabingwa.
Homa ya pambano, Yanga wajibiwa na Azam kwa staili hii... Homa ya pambano, Yanga wajibiwa na Azam kwa staili hii... Reviewed by Steve on Saturday, August 08, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.