James Rodriguez kutua Manchester United!?
Imeripotiwa kua Manchester United wataendelea na
mpango wao wa kumnasa James Rodriguez kutoka Real Madrid.
Nyota huyo amefunga mabao 17 katika mechi 46 katika msimu wake wa kwanza Real Madrid lakini amejikuta akikosa kucheza kikosi cha kwanza tangu msimu uliopita.
Rodriguez aliendelea kuwepo Santiago Bernabeu kipindi cha majira ya joto pamoja na uvumi wa kuondoka, lakini kwa sasa ipo wazi kwamba anaweza kuruhusiwa kuondoka ifikapo dirisha dogo la usajili Januari endapo klabu itakayovutiwa nae itafikia mapatano ya thamani yake.
Kwa mujibu wa Don Balon, kocha wa Man United, Jose Mourinho bado yupo katik harakati za kutafuta kiungo mshambuliaji mwingine huku akionekana kuvutiwa zaidi na Rodriguez,
James Rodriguez kutua Manchester United!?
Reviewed by Steve
on
Sunday, September 18, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment