Propellerads

Guardiola azungumzia msimamo wake wa sasa kuhusu Yaya Toure.




Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola ambaye alisema kwamba
Yaya Toure hatocheza tena kwenye kikosi chake, kwa sasa ametoa tena msimamo wake kuhusu suala hilo.

Koch huyo mhispania alimtoa Yaya kwenye kikosi chake cha UEFA msimu huu hali iliyopelekea wakala wa mchezaji huyo kutoa maoni yake.

Jumanne hii Yaya aliweka ujumbe wake kwenye Twitter akielezea furaha yake kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza na pia anavyoona ugumu wa kutopangwa kucheza.

Katika mkutano wa kablya ya mechi, Guardiola aliulizwa tena swala hilo ambapo alionekana kuchoshwa na swali hilo.

"Tunafanya nae mazoezi kila siku," alijibu kama alivyonukuliwa na ESPN.

"Lakini sizungumzii tena kesi hii. Unajua mtazamo wangu."


Guardiola azungumzia msimamo wake wa sasa kuhusu Yaya Toure. Guardiola azungumzia msimamo wake wa sasa kuhusu Yaya Toure. Reviewed by Steve on Friday, September 30, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.