Propellerads

Baada ya Allardyce, Gazeti moja laibua mazito ya rushwa EPL, wamo mameneja wakubwa, wachezaji wengine wakibett michezo yao, hatari tupu!!




Gazeti la Daily Telegraph  limedai kwamba litatoa taarifa za rushwa
kwa watu wazito zaidi Premier League ndani ya siku zijazo.

Gazeti hili tayari limetoa mkanda wa siri wa bosi wa timu ya England, Sam Allardyce ambapo ameonekana akishauri jinsi ya 'kufoji' sheria za usajili za FA kwenye umiliki wa wachezaji.

Hata hivyo wamefichua kwamba madai mazito zaidi yatafuatia ndani ya wiki moja baada ya uchunguzi wa mwaka mzima kuhusu rushwa.

Gazeti hili linadai kwamba watatoa taarifa jinsi kocha msaidizi wa klabu moja kubwa alikubali hongo ya pauni 5,000, jinsi mameneja 10 walitajwa na mawakala wa wachezaji kuchukua rushwa ili kufanya longo longo kwenye usajili na jinsi mameneja wawili maarufu walijadili ishu kama ya Allardyce.

Ripoti pia inadai kwamba wamepata taarifa kuhusu kocha mwingine mkubwa alivyofunguka mchezaji wake kuvunja sheria za FA kwa 'ku-bett' mchezo wao mwenyewe, lakini akashindwa kuripot, kwa kuongezea kiongozi mkubwa katika klabu ya Premier league akisaidia ripoti ya kuwalinda mameneja walioshiriki rushwa.

Kwa maoni na mijadala mbalimali tukutane huku KJIWE CHA SOKA bongo, usicheze mbali mtu wangu!!!

Baada ya Allardyce, Gazeti moja laibua mazito ya rushwa EPL, wamo mameneja wakubwa, wachezaji wengine wakibett michezo yao, hatari tupu!! Baada ya Allardyce, Gazeti moja laibua mazito ya rushwa EPL, wamo mameneja wakubwa, wachezaji wengine wakibett michezo yao, hatari tupu!! Reviewed by Steve on Wednesday, September 28, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.