Propellerads

Van Persie: Kwanini niliondoka Man United




Mshambuliaji wa Fenerbahce, Robin van Persie, amefichua kwanini aliamua kuondoka
klabuni Manchester United.

Mshambuliaji huyo wa kidachi alikamilisha uhamisho wake katika klabu hiyo ya Uturuki baada ya kuhofia kua anaelekea kupoteza nafasi yake kikosi cha kwanza Old Traford.

Van Persie amefichua haya baada ya kuacha benchi kwenye mechi dhidi ya Chelsea ambayo walipoteza kwa 1-0, na hapo ndipo alipofikiria mambo yameanza kubadilika.

"Hiyo ilikua ni moja ya ishara kua mambo hayaendi sawa" aliiambia Sunday Times kuhusiana na mechi ya Chelsea.

"Niliomba kucheza reserve, kupata dakika zaidi, lakini nilikaa benchi tu"

"Hali ilibadilika kati yangu na Louis na watu klabuni waliliona hilo, lakini nilikua proffesional.Kwa wakati huo sikufikiria kuondoka. (mke wangu) Bouchra alikua na furaha, watoto walikua na furaha, nilikua na furaha Manchester United"

Van Persie alizidi kufunguka kua kocha van Gaal alibadili maamuzi ya yeye kucheza kikosi cha kwanza na kumpeleka kikosi cha pili, hali iliyompelekea yeye kuamua kuhama.

"Mimi ni mchezaji mzoefu, sio mjinga.Sikukasirika. Haya mambo ni sehemu ya mpira, sehemu ya maisha. Unatakiwa ujitahidi kulingana na hali, kwa hiyo nilifanya hivyo kwa kuamua kuhama"
Van Persie: Kwanini niliondoka Man United Van Persie: Kwanini niliondoka Man United Reviewed by Steve on Sunday, July 19, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.