Steven Gerrard afichua mchezaji aliyekua anamkubali kikosini
Mkongwe wa Liverpool, Steven Gerard amefunguka kua ni mchezaji gani akimkubali zaidi
katika timu zote alizocheza, yaani timu ya taifa na klabu.
Nyota huyo mpya wa La Galaxy amepata kua kikosi kimoja na nyota wakubwa kama vile Javier Mascherano , Xabi Alonso na Fernando Torres katika ngazi ya klabu na David Beckham na Wayne Rooney kwa England.
Hata hivyo yeye anamkubali zaidi nyota wa Barca, Luis Suarez kua ni mchezaji mkali aliyepata kucheza nae.
"Alikua ni mchezaji mzuri, naweza kusema mkali zaidi kwa niliopata kucheza nao" aliiambia tovuti rasmi ya Barcelona.
" Ni mtu mzuri , mwanafamilia nje ya uwanja, tulikua pamoja muda mwingi na tulisaidiana sana katika career yetu, ndio ni rafiki yangu mzuri"
Pia Gerrard aliizungumzia pia klabu ya Barcelona na kusema kua ni klabu nzuri ndio maana wamechukua ubingwa wa Ulaya, Gerrard akiwa na timu yake mpya ya La Galaxy wataumana na Barcelona Jumatano hii asubuhi katika International Champions Cup.
Steven Gerrard afichua mchezaji aliyekua anamkubali kikosini
Reviewed by Steve
on
Tuesday, July 21, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment