Headlines za usajili magazeti ya Ulaya leo Jumapili.
Meneja wa Man United, Louis van Gaal, yuko katika harakati za kumnasa
kiungo wa Real Madrid, Gareth Bale kwa dau linalokadiriwa kufikia pauni mil 96 (Sunday People)
Winga wa Red Devils, Angel Di Maria, anaweza kuondoka klabuni hapo kuelekea Paris Saint-Germain msimu huu, lakini mmamuzi yote yako chini yake. ( Mail on Sunday)
Bosi wa Chelsea, Jose Mourinho, amewaambia Everton bado ana nia ya kumnasa mlinzi John Stones, 21, japokua ofa yake ya kwanza ya pauni mil 20 kukataliwa ( Sunday Mirror)
Mourinho amesema kikosi chake kilichochukua ubingwa mwaka jana hakihitaji marekebisho makubwa sana, japo amewaeleza wachezaji kuperfom zaidi kuliko msimu uliopita ( Observer)
Kiungo wa Chelsea, Oscar, 23, amesema hana mpango wa kujiunga Juventus japokua amekua akihusishwa sana na mabingwa hao wa Italy ( London Evening Standard)
Tottenham wamepanga wiki hii kumtengea kiasi cha pauni mil 15 mshambuliaji wa w
West Bromwich, Said Berahino ( Sunday People)
West Bromwich wanajiandaa kukamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa Liverpool, Rickie Lambert, 33 ( Birmingham Mail)
Aston Villa wanataka kufanya uhamisho utakaogharimu kiasi cha pauni mil 7 kwa mshambuliaji wa Bournemouth, Callum Wilson, 23, ili kuziba pengo la Benteke ( Sunday Express )
Ripoti nyingine zinadai kua, Aston Villa wanataka kutumia pesa waliyomuuzia Benteke kiasi cha pauni mil 32.5 kumuwania mshambuliaji wa QPR na timu ya England, Charlie Austin ,26 ( Sunday Mirror )
Newcastle na Leicester pia nao wako katika mbio za kumnasa Austin ( Star on Sunday)
Headlines za usajili magazeti ya Ulaya leo Jumapili.
Reviewed by Steve
on
Sunday, July 19, 2015
Rating:
